VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Thursday, February 19, 2015

LORI LA MAFUTA LAUA NA KUJERUHI TENA MBEYA


WATU WAWILI 1. MARIA PAJELA [18] NA 2. WILLIAM S/O PASCHAL [38] ,WOTE WAKAZI WA KIJIJI  CHA IDWELI, KATA YA ISONGOLE, TARAFA YA UKUKWE WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA, WALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUUNGUA MOTO KIJIJINI HAPO JANA.


TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI LEO, IMESEMA KUWA, KATIKA TUKIO HILO MAREHEMU HAO PAMOJA NA BAADHI  YA WANANCHI WENGINE WA KIJIJI HICHO WALIKUWA KATIKA HARAKATI ZA KUIBA MAFUTA KUTOKA KATIKA GARI T.891 AQZ /T.821 ARF AINA YA SCANIA MALI YA AILIS SANGA LILILOKUWA LIMEBEBA MAFUTA AINA YA PETROLI UJAZO WA LITA 41,000, LIKITOKEA DSM KUELEKEA NCHINI MALAWI,  LIKIENDESHWA NA DEREVA ZAWADI NYATO [46] MKAZI WA SAE MBEYA AKIWA NA TINGO WAKE FRANK YOHANA [24],MKAZI WA MBOZI.

AWALI KABLA YA TUKIO HILO GARI HILO LILIACHA NJIA NA KUPINDUKA, HIVYO WAHANGA [DEREVA NA TINGO] WALIFANIKIWA KUOKOLEWA NA KUPELEKWA KITUO CHA POLISI KIWIRA ILI KUPATA HATI YA MATIBABU [PF3] KWA AJILI YA KWENDA HOSPITALINI KUPATIWA MATIBABU. HATA HIVYO BAADHI YA WANANCHI WA ENEO HILO WALIVAMIA GARI HILO NA KUFANIKIWA KUTOBOA TANKI LA MAFUTA, HALI ILIYOPELEKEA MAFUTA KUANZA KUMWAGIKA/KUSAMBAA MAENEO HAYO NA HATA KUELEKEA MAENEO YENYE MAKAZI YA WATU  NA WAO KUKINGA KWA KUTUMIA VYOMBO VYAO.


KATIKA TUKIO HILO WATU KUMI NA NANE [18] WALIJERUHIWA, KATI YAO WANAUME NI 13 NA WANAWAKE 05 AMBAO NI: 1. SHUKURU KANZALE [21], 2. NURU GEORGE [30], 3.ASANTE BONIFACE [38], 4. JOSEPH JAMSON [18], 5.JOSEPH PASCHAL [30], 6.SIZA KANESA [22], 7.ALEX  DAUD [35], 8. OSCAR YOSIA [23], 9.TRAIPHON MOASI [37], 10.SAMSON MBWILA [29].

WENGINE NI 11. DORA MICHAEL [35],12. VERONICA ELIA [30],13.RABSEN AYUB [26], 14.WASIWASI SPIKA [32], 15.ASIA ANON [20], 16.BAHATI KYANDO [23], 17. CHRISTOPHER ERASTO [32] NA 18. MELISA SANANE [50], WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA IDWELI. AIDHA KATI YA MAJERUHI HAO,MAJERUHI 16 WAMELAZWA HOSPITALI YA MISHENI –IGOGWE NA MAJERUHI WAWILI WAMELAZWA HOSPITALI YA SERIKALI MAKANDANA-TUKUYU NA HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI.

No comments: