VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Tuesday, March 31, 2015

MAUAJI TENA: Mfanya biashara Arusha adaiwa kumuua rafiki yake


MFANYABIASHARA maarufu wa madini ya tanzanite jijini Arusha, Felix Mmasi (41) anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha akituhumiwa kumpiga risasi kwa kutumia silaha aina ya bastola mtu anayedaiwa kuwa ni rafiki yake na kumsababishia umauti. 

Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas alipoulizwa na mwandishi wa gazeti hili juu ya kuwepo kwa tukio hilo. 

Sabas alikiri Polisi kumshikilia mtuhumiwa huyo, lakini alisema taarifa rasmi ya tukio hilo atazitoa leo kwa waandishi wa habari mara baada ya kuchukua maelezo kwa mtuhumiwa. 

Katika Kituo Kikuu cha Polisi, wafanyabiashara wa madini na watu wengine walimiminika kumshuhudia mwenzao, huku wengine wakionekana kutafuta njia za kutoa kila aina ya msaada kwa mwenzao.

No comments: