VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Tuesday, March 31, 2015

Wafanyabiashara wa Daladala Songea Wagoma Kufanya Kazi Zao Kwa Madai ya Kuunga Mkono Mgomo wa Wafanyabiashara Unaoendelea.


Mgomo wa wafanya biashara umeendelea kuchukua sura mpya baada ya wafanya biashara wa daladala mjini Songea kugoma kufanya kazi toka asubuhi kwa madai ya kuunga mkono mgomo wa wafanya biashara unaoendelea katika mikoa mabalimbali nchini ili kushinikiza serikali kumuachilia kiongozi wao Bwana Joseph Minja pamoja na kutatua madai yao ya matumizi ya mashine za EFDS pamoja na ongezeko la kodi kwa asilimia mia moja.
 
Kwa mujibu wa mwandishi wetu aliyepo mjini songea hali hiyo imesababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wa songea ambao wamelazimika kutembea kwa miguu kwenda maeneo mbalimbali ya mji huo ambapo jeshi la polisi limeimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya mji huo.
Wakati  hayo  Yakijiri,Naibu Spika wa Bunge  leo ameiagiza Kamati ya Uongozi kukutana na serikali kutafuta suluhu ya suala la mgomo wa wafanyabiashara unaoendelea nchini.

No comments: