VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Friday, October 31, 2014

Taarifa nyingine kuhusiana na kuanguka kwa kanisa la T.B Joshua

Synagogue-Collapse-BellaNaija1

Serikali ya jimbo la Lagos Nigeria, imesema sehemu ya jengo lililoaanguka katika kanisa la
Synagogue Church of All Nations, ambalo lilijengwa kwa ajili ya kufikia wageni lilijengwa bila kibali cha Serikali.
Kamishna anayesimamia mipango miji Lagos, Olutoyin Ayinde 
 
Amesema uchunguzi uliofanywa na tume iliyoongozwa na Oyetade Komolafe umeonyesha hakuna kibali kilichotolewa na 
 mamlaka hiyo kuidhinisha ujenzi wa jengo la ghorofa sita.
 
Amesema kibali kilichotolewa kilikuwa cha ujenzi wa jengo la kanisa ambalo ni ukubwa wa ghorofa tano pekee, na uchunguzi umebaini kibali hicho kilikiukwa kwa kujengwa ghorofa nane badala ya tano.

Anyinde amesema mamlaka hiyo imeagiza mamlaka ya anga kuchunguza juu ya ndege ambayo imedaiwa kuzunguka jengo hilo muda mfupi kabla ya jengo kuanguka.

tb-joshua 
Kesi hiyo inayosikilizwa mahakama kuu Lagos imeahirishwa mpaka Novemba 5 ambapo T.B Joshua atatoa ushahidi. Jengo hilo lilianguka Septemba 12 na kuua watu 116.

No comments: