VITUS BENEDICTO MTAFYA

SPORT AND GAMES

Friday, October 31, 2014

YANGA KUIVAA KAGERA KESHO


  Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezini leo asubuhi katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba
  
  Kikosi cha timu ya Young Africans kesho (jumamosi) kitashuka dimbani kusaka pointi tatu muhimu kutoka kwa wenyeji timu ya wakata miwa Kagera Sugar mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
      Msafara wa Young Africans uliwasili jana mchana mjini Bukoba na kufanya mazoezi jioni katika Uwanja wa Kaitaba kabla ya kupumzika na leo asubuhi kufanya mazoezi mepesi ya mwisho kabla ya mtanange huo.
Kocha Marcio Maximo mara baada ya mazoezi ya leo asubuhi amesema anashukuru vijana wake wote wapo fit kuelekea kwa mchezo huo wa kesho ambao anaamin utakua mgumu kutokana na ubora wa timu ya Kagera Sugar lakini atapambana kuhakikisha anapata pointi tatu muhimu.
"Nimekua nikiifahamu Kagera Sugar kwa muda mrefu sasa, tangu nikiwa kocha wa timu ya Taifa (Taifa Stars) wamekua wakitoa upinzani kwat kubwa za Ligi Kuu lakini mie pamoja na jeshi langu tumejipanga kuhakikisha tunafaya vizuri kwa kupata pointi tatu" alisema Maxim.
Aidha Maximo amesema kuelekea katika mchezo wa kesho atawakosa washambuliaji wake wawili (Msuva & Javu) amabo ni majeruhi lakini wachezaji wengine 26 waliobakia wote wako fit kuelekea kwenye mchezo huo.
Young Africans inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa kuwa na pointi kumi (10) sawa na timu ya Azam inayoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa huku Mtibwa Sugar ikiongoza Ligi kwa pointi 13.

No comments: