Al Shabaab wakiri kuwaua 36 KenyaKundi la wanamgambo nchini Somalia Al Shabaab limekiri kuwaua watu 36 katika shambulio lililotokea kwenye machimbo ya kokoto karibu na mji wa Mandera kaskazini mwa Kenya. Katika taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa kundi hilo, wanamgambo hao wamesisitiza kuwa ndio waliowaua wakenya hao kwa sababu ya majeshi ya Kenya kuendelea kuwa nchini Somalia. Taarifa za mauaji hayo zilitolewa kwa mara ya kwanza na Shirika la Msalaba Mwekundu. Wakazi wa eneo hilo wamesema waathirika wote wa tukio hilo ni watu wasio Waislam ambao walikuwa wakifanya kazi katika machimbo hayo yaliyopo Kormey kilomita 15 kutoka mji wa Mandera Kaskazini mwa Kenya. Tukio hili linafuatia tukio la wiki moja iliyopita ambapo watu wapatao 28 waliuawa katika shambulio la basi la abiria huko Mandera.
Wapiganaji wa Al Shabaab
Kundi la wanamgambo nchini Somalia
Al Shabaab limekiri kuwaua watu 36 katika shambulio lililotokea kwenye
machimbo ya kokoto karibu na mji wa Mandera kaskazini mwa Kenya.
Katika
taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa kundi hilo, wanamgambo hao
wamesisitiza kuwa ndio waliowaua wakenya hao kwa sababu ya majeshi ya
Kenya kuendelea kuwa nchini Somalia. Taarifa za mauaji hayo zilitolewa kwa mara ya kwanza na Shirika la Msalaba Mwekundu. Wakazi
wa eneo hilo wamesema waathirika wote wa tukio hilo ni watu wasio
Waislam ambao walikuwa wakifanya kazi katika machimbo hayo yaliyopo
Kormey kilomita 15 kutoka mji wa Mandera Kaskazini mwa Kenya. Tukio
hili linafuatia tukio la wiki moja iliyopita ambapo watu wapatao 28
waliuawa katika shambulio la basi la abiria huko Mandera.
Kundi la wapiganaji wa Kiislam la Al Shabab wamekiri kuhusika na mauaji hayo. Mkuu wa Polisi hilo amesema bado wanafuatilia tukio hilo. Katika
tukio lingine, mtu mmoja ameripotiwa kuuawa nchini Kenya kufuatia
mlipuko katika klabu moja ya usiku katika mji wa Wajir kaskazini mwa
Kenya.
Basi walimokuwa wakisafiria wakenya wengine waliouawa na Al Shabaab mjini Mandera wiki iliyopita
Kwa mujibu wa Kamishna wa
Polisi wa Wajir, Frederick Sishia, shambulio hilo limefanyika saa mbili
usiku na kuua mtu mmoja na watu wengine wanne wamejeruhiwa. Washambuliaji hao walitumia magruneti na silaha nyingine za kijeshi kufanya shambulio hilo. Wiki iliyopita watu wengi waliuawa eneo la Mandera kaskazini mwa Kenya. Kenya
imejikuta ikilengwa na mashambulio ya kigaidi tangu majeshi yake
yapelekwe nchini Somalia kukabiliana na wapiganaji wa Al Shabab. Mbali
na miji ya kaskazini mwa Kenya kushambuliwa kila mara, miji mikubwa
nchini humo ya Nairobi na Mombasa imekuwa ikilengwa na mashambulio ya
kigaidi.
No comments:
Post a Comment