Wanachama wa chama cha maalbino wakitembelea kisiwani ambako wanaishi walemavu wa ngozi
Mtobi
Namigambo, ni mvuvi anayeuza samaki, amekaa kwa utulivi nje ya nyumba
yake ya matope katika kisiwa cha ukerewa mahali ambapo zamani palikuwa
makao ya albino lakini kwa sasa si hivyo. Mtoto wake wa miaka nne May
Mosi ameketi kwenye paja lake akionyesha umarufu wake wa hisabati kwa
kuhesabau moja hadi kumi kwa ujasiri.
Mara kwa mara Mtobi
anamtazama mke wake, Sabina, ambaye ameketi kwa mkeka kando yake
akitayarisha chakula cha jioni. Watoto wake wengine wawili wanachezea
hapa karibu na pia wamejaliwa na mtoto mchanga amabye yuko chumbani
analala.
May alipokuwa na umri wa miezi mitatu, aliponea jaribio la kutekwa nyara.
Albino wanauawa kinyama kwa ajili ya imani potovu
" nilikuwa nimeenda ziwani
kuvua samaki. walikuwa pekee yao nyumbani wavamizi walipokuja, mke wangu
alitorokea kwa dirisha na kukimbillia usalama akiwa na May, na
akawawacha watoto hawa wawili nyumabani ambao hawakuwadhuru kabisa",
Mtobi ananiarifu.
"Wavamazi hao walikuwa wakimtaka May," Sabina
anaongezea, "mume wangu alikuwa ameenda safari ya uvuvi na wavamizi hao
walijua na hio ndio sababu walikujia mtoto wangu, baada ya kutorokea kwa
dirisha, bado waliniandama huku nikipiga mayoye ya usaidizi, waliwacha
kuniandama wakati tu niliwaamsha majirani"
May ni mojawapo wa
Albino sabini wanaoishi katika kisiwa hiki cha Ukerewa ambacho ni masaa
matatu tu kutoka mwanza, mji wa pili mkubwa zaidi Tanzania. Elimu kwa jamii
Mtobi
anasema "tunaiomba serikali kufanya juhudu zaidi za kuelimisha jamii
hapa, serikali ishawahi kuandaa majadiliano kuhusu Albino na kulikuwa na
mabadiliko makuwa, akini si hivyo tena"
Shirika lisilo la
kiserekali chini ya mrengo wa 'The Same Sun' linalowashughulikia jamii
ya Albino hapa Ukerewa, linasema kuwa kisiwa hiki hakina usalama kando
na vile watu wangependa kuamini.
Idadi ya maalbino waliouawa ni kubwa na kuna hofu ya wengine wengi kuuawa kutokana na imani potovu
Mwenye kiti wa chama cha
maalbino tawi la Mwanza, (TAS) Alfred Kapole, mzaliwa wa Ukerewe,
alilazimika kutorokea mji wa Mwanza akiwa mmoja wa albino wa kwanza
kufika kortini baada ya kiognozi mmoja wa kijiji akitaka kumuua kwa
ajili ya nywele zake.
Mwaka uliopita boma lake lilivamiwa, kwa bahati nzuri alikuwa ameenda mwanza. Kulikuwa na jairibio lEngine la kumuua mwaka huu. Kampeni kabambe
Serikali ya Tanzania imeanzisha kampeni ili kuchangisha fedha za kuelimisha jamii.
Kampeni nyingi za uhamasishaji hufanyika mijini kwani ni rahisi kufikia watu,lakini ni vijiji ndivyo vinahitaji msaada zaidi.
Ramadhan
Khalfan, ambaye ni mwenyekiti wa chama cha albino Ukerewa,anasema kuwa
wanataka kufikia maeneo ya vijiji na kuzungumza na watu,lakini ni vigumu
kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha.''Hatuna uwezo ama njia za
kufikia jamii zilizoko vijijini.Aliongezea kusema,''tunategemea pakubwa
redio na televisheni,lakini hatuwezi kufika mashinani kwa sababu ya
gharama.''
Mnara unaowapa matumaini watanzania Serengema
Sehemu ya Serengema inapatikana
kilomita 60 (maili 33.5) kutoka Mwanza.Ili kusisitiza shida
hii,umejengwa mnara katika mzunguko katikati ya mji.
Ni sanamu ya
chuma kimo cha binadamu,inayoonyesha baba mwenye rangi akimbeba begani
mto wake albino huku mama yake mwenye rangi akitundika kofia yenye
ukingo mpana kwenye kichwa cha mwana huyo kumkinga kutokana na miale ya
jua.Pia kuna majina ya watu 139 ya waathiriwa waliouawa,kuvamiwa ama
miili yao kuibiwa kutoka kwenye makaburi.
Serengema ndio sehemu iliyoathirika vibaya zaidi.
Kuna
mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi pamoja na chama
cha Tanzania Albino katika kuhamasisha na pia kujenga makaazi.
Mashirika yasiyo ya kiserikali yanaamini kuwa uhamasisho na kuacha imani potovu zinaweza kusimamisha mauaji haya.
Kamanda mkuu wa polisi mjini Mwanza anasema kuna
changamoto nyingi sana katika kukabiliana na mauaji ya Albino
Mwakilishi wa chama cha
Serengema Mashaka Benedict anasema kuwa watu bado wanaamini kuwa sehemu
za mwili wa albino zinaweza kuleta utajiri.''Kama hiyo ndiyo hali,mbona
sisi si matajiri?''anauliza.
Anadai kuwa watu mashuhuri wanahusika
katika ''biashara ya mauaji'' na ndio maanake watu wachache sana
wamekamatwa,kushitakiwa,kupatikana na hatia ama kufungwa.''Itakuwa vipi
masikini kutoa dola 10,000 kwa kipande cha mwili?,ni wanabiashara na
wanasiasa ndio wanaohusika.''
Hata hivyo polisi wanasema kuwa
wanachungunza kila moja ya visa lakini wanakosa ushahidi wa kuthibitisha
madai yanayotolewa.Kamanda wa polisi wa Mwanza,Valentino Mlolowa
anasema,''Kesi hizi ni ngumu kwa kuwa visa hufanyika mashinani sana
katika sehemu ambazo hazina stima kwa mfano,na hiyo inafanya kuwajua
wahalifu usiku kuwa vigumu.Tunachunguza kila moja ya kesi na
madai,lakini kama uonavyo,si
rahisi.''
Yaweza onekana kama kuwa
tumepoteza kila kitu lakini hii haiwazuilii watu wanaoishi na hali ya
Uhalbino kama May Mosi,kutokuwa na tumaini kuwa fedha zinazochangishwa
kutoka kwenye kampeni iliyoanzishwa na serikali zitasaidia kusikizwa
zaidi kwa Albino nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment