Baada ya kupiga Collabo na Miss Trinity katika studio za B-Hits, weekend
hii Ambwene Yesaya a.k.a A.Y amefichua siri ya kupiga Collabo na
Wasanii mbalimbali wa kimataifa wanaoshuka bongo kila kukicha. A.Y
ameyasema hayo baada ya kuulizwa na swali 255 kwamba ni mbinu gani
anayoitumia katika kumshawishi mtu kama Sean Kingston, P-Square, Miss
Trinity, K-Naan na wengineo.
Ambwene akajibu kuwa siri yake ya
mafanikio hayo ni kujitangaza sana kupitia vyombo mbalimbali vya habari
kadri inavyowezekana, so anapokuja msanii kutoka nje Tayari wanakua
wameshafanya utafiti wa kujua ni msanii gani mkali au anayejulikana
nchini Tanzania.
Ambwene pia amezungumzia Collabo yake na Sean Kingston ambayo
walishindwa kuifanya hapa bongo na meneja wa Kingston akamshauri Ambwene
kuwa ili aweze kujitangaza zaidi ni bora aende kurekodi nchini marekani
kwani atapata fursa ya kukutana na wataarishaji wa muziki wa kimataifa
lakini pia kazi atakayofanya na Kingston itakua yenye ubora.
A.Y yuko mbioni kwenda katika mji wa Miami nchini marekani kurekodi ngoma na mtu mzima Sean Kingston.
Lakini pia kesho A.Y anaelekea jijini Kampala kupiga Video ya ngoma aliyorekodi na Miss Trinity.
No comments:
Post a Comment